Saturday, November 29, 2014

MAAZIMIO YA BUNGE JUU YA SAKATA LA ESCROW

Baada ya Sakata la ESCROW kuchukua muda mrefu katika mijadala wa vikao vya Bunge hatua iliyopelekea Bunge kuweka historia ya kuendelea na kikao chake jana tarehe 28/11/2014 hadi saa tano Usiku. Aidha katika kikao hicho hakikumalizika kwa hali nzuri kutoka na na Baadhi ya wabunge wa CCM kuonekana waziwazi wakiwatete Watuhumiwa wa wizi wa mabilioni ya fedha za ESCROW.

Katika hatua nyingine leo tarehe 29/11/2014 iliundwa kamati maalum iliyojumuisha PAC, CCM na UKAWA ambapo kwa niaba ya Bunge walifikia maazimio yafuatayo ambayo baadaye saa 7:00 Jion yalisomwa Bungeni na kuridhiwa na wabunge walio wengi.

1.BUNGE LINAAZIMIA KUWA WOTE WALIOHUSIKA WAWAJIBIKE NAKUWAJIBISHWA KWA MUJIBU WASHERIA

2.SERIKALI IANGALIE UWEZEKANO WA KUTAIFISHA NA KUFANYA MITAMBO YA IPTL SASA IMILIKIWE NA SERIKALI

3.SERIKALI IPITIE UPYA MIKATABA YOTE NA KUANGALIA KAMA INAMASLAHI NA TAIFA,NA IBORESHWE.

4.SERIKALI ILETE MUSWADA WAKUREKEBISHA SHERIA YA TAKUKURU ILI KUUNDA CHOMBO KINGINE KITAKACHOKUWA NA NGUVU ZAIDI YA KUPAMBANA NA RUSHWA KUBWA KUBWA

5.MAJAJI WALIOTAJWA KUHISIKA INAPENDEKEZWA KUWA MH RAIS AUNDE TUME YA KIJAJI KUWACHUNGUZA JAJI ALOIS NA JAJI LUHANGISA NA KISHA WACHUKULIWE ATUA

6.BANK YA STANBIC BANK TZ LTD NA BANK NYINGINE ZOTE ZILIZOHUSIKA KATIKA KUTAKATISHA PESA HARAMU ZA KAMPUNI ZA (PAP NA VIP LTD) NI JINAI NA BANK HIZO ZOTE ZITANGAZWE NA MAMLAKA HUSIKA KUWA NI BANK ZENYE SHAKA YA UTAKATISHAJI NA UPOKEAJI WA PESA HARAMU

7.BUNGE LINASHAURI NA KUAZIMIA WAZIRI WA MADINI, WAZIRI WA ARDHI,MWANASHERIA MKUU,KATIBU MKUU WA WIZARA YA NISHATI NA MADINI,WAWAJIBISHWE NA MAMLAKA YA UTEUZI ITENGUE UTEUZI WAO.

8.WENYEVITI WA KAMATI ZA BUNGE AKIWAMO MH NGELEJA WANAOTAJWA KUHUSIKA WAVULIWE UENYEKITI NA NAFASI ZAO KAMATI HUSIKA ZICHUKUE HATUA HARAKA KUWAVUA NAFASI ZAO

Nawapongeza wabunge wote kwa kuondoa tofauti zao na kujali maslai ya taifa!!!!!

No comments:

Post a Comment