CHADEMA WAANZISHA MGOGORO NA BODABODA IRINGA MJINI
Ni siku mbili tu zimepita toka tarehe 23/08/2014 mh Mwigulu Nchemba Naibu Katibu mkuu CCM Bara na Naibu Waziri wa Fedha alipomuapishwa komredi Salim Abri (ASAS) kuwa Kamanda wa UVCCM mkoa wa Iringa na baadae kuhutubia mkutano mkubwa wa kihistoria wa hadhara katika viwanja vya Mwembetogwa Iringa mjini.
Sherehe hizo zilishirikisha wanaCCM wengi sana wa ndani ya mkoa wa Iringa na nje,Wananchi wengi sana kutoka takribani kila kata ya Manispaa ya Iringa.Pia vijana waendesha Bodaboda kutoka vijiwe mbalimbali nao walishiriki kikamilifu kuanzia mapokezi ya Mh Mwigulu Nchemba,kumsindikiza mitaani katika ufunguzi wa mashina ya Wakereketwa na baadae kumsindikiza kwa furaha kubwa na mbwembwe nyingi hadi eneo lililofanyika mkutano.
Vijana hawa wa Bodaboda wamekuwa wakikabiliwa na matatizo na chamgoto nyingi kwenye kazi zao za kila siku na kila wanapomfuata mbunge wao waliemchagua Mch Peter Msigwa amekuwa akiwapa majibu ya dharau,kejeli na kebehi kuwa hana nafasi,ana majukumu mengi ya chama chake au hana fedha na mara nyingi huwaambia kuwa jukumu la kuwasaidia sio la kwake,hiyo ni kazi ya CCM iliyo madarakani.
CCM iliamua kubeba jukumu la kufanya kazi alizokataa mbunge huyo la kuhangaika kutatua matatizo na changamoto zinazowakabili vijana hao wa Bodaboda,ikiwa ni kwanza kuwasaidia kuunda umoja wao,kufanya uchaguzi wa kidemokrasia ili kupata viongozi wao,kufanya mazungumzo na viongozi wa Sumatra,Polisi na Halmashauri ya Manispaa kuweka mpango mzuri wa kufanya kazi zao bila kubughudhiwa na vyombo hivyo kama awali ambapo walikuwa wanafanya kazi katika mazingira magumu sana ya kukimbizana na maafisa hawa.
Pia CCM inapambana kuwatafutia mikopo na wafadhili wa kuwasaidia mitaji,akiwemo Kamanda wa UVCCM mkoa Salim Abri(ASAS) ambae amekuwa msaada mkubwa sana kwao katika shida zao mbalimbali.
Kwa kazi nzuri inayofanywa na viongozi wa CCM kuwajali na kupambana katika kushughulikia matatizo yao,vijana hawa kwa hiari yao waliamua kuwa karibu na CCM na kusaidia kufanikisha kazi mbalimbali za CCM,kama walivyofanya tarehe 23/08/2014 katika kuapishwa kwa Kamanda na katika mkutano wa mh Mwigulu Nchemba.
Kitendo cha vijana hawa kushiriki kikamilifu katika mkutano wa CCM wa mh Mwigulu Nchemba wa juzi tarehe 23/08/2014 kilionekana wazi kumkera sana mbunge Mch Peter Msigwa kwa kuona kuwa vijana wameamua kumsaliti na amehisi kuwa anazidi kupoteza kundi kubwa na muhimu la vijana ambalo awali lilikuwa likimuunga sana mkono likiamini labda angewaletea miujiza katika maendeleo na kumbe wakaishia kashfa na kutelekezwa.
Leo tarehe 25/08/2014 Bw.Msigwa akaitisha mkutano wa vijana hao wa Bodaboda katika ukumbi wa Walfare,akiwa na malengo yafuatayo:-
-Kwanza kuwajenga chuki dhidi ya CCM kwa kuwachonganisha kwa fitina kuwa eti CCM imemnunua mwenyekiti wao na imemjengea nyumba hivyo wamkatae.
-Aliwaambia eti uchaguzi waliofanya mwanzo ni batili kwa sababu mwenyekiti waliemchagua anaonekana anaisikiliza sana CCM.
-Alitoa ahadi ya shilingi Milioni tatu na kuwa atawaletea pikipiki kumi ifikapo mwezi Februari 2015 ili wafanyie kazi.
-Alitoa maagizo hapo mkutanoni kuwa mwenyekiti na viongozi wenzake wanaotuhumiwa kuitii CCM washambuliwe kwa kipigo mara moja ili iwe fundisho kwa wengine kuiunga mkono CCM.
Baada ya maelekezo hayo ya mbunge kutolewa ndipo mabaunsa wa Chadema walipoanza kufunga milango ya ukumbi ili kipigo kianze.Wale viongozi walifanikiwa kutoka nje wakikimbia na nyuma wakiandamwa na wafuasi wa Mch Msigwa na mabaunsa.
Pale nje ya ukumbi walikuwepo vijana wengine wengi wa Bodaboda ambao walizuiwa na mabaunsa kuingia ukumbini kwa madai kuwa ni vibaraka wa CCM.Vijana hawa walipoona viongozi wao wanakimbizwa na kushambuliwa,nao waliamua kuingilia kati kuwatetea.
Vurugu zilikuwa kubwa na ziliendelea kwa muda kidogo hadi Polisi walipofika eneo la tukio na kujaribu kutuliza bila mafanikio hadi walipoamua kupiga risasi kadhaa angani ndio vurugu zikatulia.
Polisi walipouliza nini kimetokea?walipewa maelezo na Bw. Msigwa kuwa huyo kijana ametumwa na CCM kuja kufanya fujo ili avuruge mkutano wao.Polisi walimchukua mwenyekiti huyo wa Bodaboda kwa kwenda nae kwa madai kuwa anaenda kuandika maelezo kituoni na baadae ataachiliwa huru.
Bw. Msigwa aliwaagiza vijana hao wakutane baada ya wiki mbili na kuwaondoa madarakani hao viongozi wanaoonekana kuiunga mkono CCM na yeye atasimamia ili wachaguliwe viongozi wengine ambao wataweza kupambana na CCM.
Mwisho kabisa kila aliyeshiriki kikao alipata Soda moja na fedha shilingi elfu tano.
Kuanzia hapo umejitokeza mgawanyiko mkubwa kati ya kundi la wanaomuunga mkono mch Msigwa kwa ushabiki, urafiki na posho ya shilingi elfu tano,na wale wanaodai kuwa hawawezi kuiacha CCM maana ndio mtetezi wao wanapokuwa na matatizo.
************MWISHO*************
No comments:
Post a Comment